Mamlaka za usalama nchini Ukraine, zinasema zimezuia mashambulizi ya makombora 15 kati ya 18 ya Urusi yaliyokuwa yamepangwa kushambulia mji mkuu wa nchi hiyo Kyiv na kwamba watu 34 walijeruhiwa wakiwemo watoto watoto.

Kwa mujibu wa ripoti ya mamlaka hiyo iliyochapishwa kwenye ukurasa rasmi wa Twitter wa mamlaka hiyo, ilisema kuwa kuna picha zinazoonyesha kuwa Russia imefanya juhudi maalum ili kuimarisha mpaka wa kaskazini wa eneo inalolikalia kimabavu la Crimea, “ikiwemo eneo lenye ulinzi karibu na kijiji cha Medvedevka.

Aidha, taarifa ya Wizara ya ulinzi nchini humo pia nayo imesema Urusi imechimba mahandaki katika eneo la mamia ya maili ndani ya mpaka wa wake unaotambuliwa kimataifa, ikiwemo mikoa ya Belgorod na Kursk kama njia moja wapo ya kuongeza ulinzi wa kukalia eneo hilo kimabavu.

Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Ukraine, imesema mshambulizi ya Urusi nchini humo yameua watoto wasiopungua 477 na kuwajeruhi watu 1,000 tangu kufanyika kwa uvamizi zaidi ya mwaka mmoja uliopita.

Waliofutiwa matokeo kurudia mtihani
Washambuliaji watano wasakwa Man Utd