Shauri jipya la kikatiba linalohusu Uraia pacha lililofunguliwa na Raia sita wa Marekani, Uingereza na Canada wenye asili ya Tanzania ambao ni Shaban Fundi, Patrick Nyelesa Nhigula, Restuta Kelemera, Njole Muya, Emmanuel Emmanuel na Bashir Kassam, leo February 20 2023 limetajwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala ya Kivukoni.

Shauri hilo namba 18 la mwaka 2022 lilifunguliwa December 16,2022 na Raia hao dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kupitia Wakili wao Peter Kibatala ambapo Raia hao waliondoka nchini na kwenda ughaibuni kwa nyakati tofauti hasa katika Nchi za Marekani, Uingereza na Canada ambako wanaishi na kufanya kazi huko baada ya kupata Uraia wa Nchi hizo.

Katika shauri hilo Raia hao wanaiomba Mahakama itamke kuwa vifungu vya sheria ya Uraia vinavyozuia Uraia pacha ni batili huku wakidai kuwa vifungu hivyo vinakiuka haki zao za kikatiba kwa kuwa vinawanyang’anya haki ya asili isiyonyang’anyika kwa maana ya Uraia wa kuzaliwa ambapo vifungu vyenyewe ni kifungu cha 7(1) na (2) (c), (4) (a) (6) vya sheria ya Uraia.

Raia hawa pia kupitia kiapo chao Mahakamani wamedai kuwa wanaathirika na kitendo cha kunyimwa haki mbalimbali katika Nchi yao waliyozaliwa kwa kuzingatia kwamba walipata uraia wa Nchi hizo kwa sababu tu za kutafuta maisha lakini mapenzi yao kwa Nchi walimozaliwa yako palepale.

Utaratibu kuingia Stendi ya Magufuli wabadilika
Kimbunga: TMA yawatoa hofu Watanzania