Marekebisho ya mkataba wa kimataifa, wa kuzuia uchafuzi utokanao na usafiri wa meli (MARPOL) kiambatisho VI umeanza kutumika rasmi kuanzia mwezi Novemba 2022. 

Sheria hiyo, iliundwa chini ya mfumo wa mkakati wa awali wa shirika la kimataifa la usafiri wa majini IMO, ukiwa na lengo la kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa GHG, kutoka kwenye safari za meli na kukubaliwa mwaka 2018. 

Marekebisho hayo ya kiufundi na kiutendaji, yanahitaji meli kuboresha ufanisi wa kinishati katika muda mfupi na hivyo kupunguza utoaji wa gesi chafuzi au hewa ukaa ili kuwa kichocheo cha kupunguza kasi ya uzalishaji wa hewa ukaa itokanayo na safari za meli zote kwa asilimia 40% ifikapo 2030.

Sheria hiyo, iliundwa chini ya mfumo wa mkakati wa awali wa shirika la kimataifa la usafiri wa majini IMO, ukiwa na lengo la kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa. Picha: theguardian.

Katibu mkuu wa IMO, Kitack Lim amesema, “Hatua za muda mfupi za kupunguza hewa ukaa (GHG) zilizopitishwa mwaka 2021, zinaunda seti kamili ya marekebisho ya MARPOL Annex VI, ambayo hutoa vizuizi muhimu vya mbinuza hatua za baadaye za IMO za kupunguza hewa chafuzi katika kipindi cha muhula wa kati.” 

Lim meongeza kuwa, kuondoa hewa ukaa katika usafirishaji wa meli za kimataifa ni suala la kipaumbele kwa IMO na “sote tumejitolea kuchukua hatua pamoja katika kurekebisha mkakati wetu na kuimarisha azma yetu. 

Marekebisho hayo, yanajengwa juu ya hatua za ufanisi wa nishati za IMO ambazo zilipitishwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 2011 na kuimarishwa tangu hatua za CII na EEXI ili kufikia malengo yaliyowekwa katika mkakati wa awali wa IMO kuhusu GHG.” 

Profesa ‘autikisa’ mjadala Nishati safi ya kupikia.
Kifo cha mtoto 'swiming pool': Polisi yawashikilia wafanyakazi wa Davido