Wizara ya Maji kwa kushirikiana na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), wamepanga kushirikiana ili kuweza kuyavuna maji ya mvua wakati wa msimu wa masika, wakilenga kufanikisha uendelezaji wa utoaji wa huduma ya maji wakati wa kiangazi.

Hayo yamebainishwa hii leo Novemba 10, 2022 na Waziri wa Maji, Juma Aweso wakati akitoa maelekezo kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye alifika kujionea jinsi uzibuaji na usafishaji wa visima vya maji vilivyokuwa vikitumika awali unavyofanyika.

Amesema, maji mengi ya mvua yamekuwa yakipotea bure wakati wa masika na kwamba kuitipia wazo hilo ni wazi kuwa watafanikisha kuondoa shida za maji zinazowakabili wananchi hasa katika vipindi vya kiangazi ambavyo huwa na ukosefu wa mvua.

Uvunaji wa maji ya mvua. Picha ya Premier petch

Waziri Aweso ameongeza kuwa, “Mheshimiwa Waziri Mkuu, kwa kushirikiana na DAWASA tutahakikisha tunalala site mpaka maji yapatikane, na nikuhakikishie tutayavuna maji ya mvua na kuyahifadhi ili kuondosha shida ya maji kwa Wananchi wakati wa kiangazi.”

Aidha, amesema ujio wa Waziri Mkuu katika kujionea harakati za uondoshaji wa shida ya maji kwa wananchi ni faraja kwa watendaji, na kwamba hali hiyo imewapa nguvu ya kupambana, ili kuhakikisha maeneo yote yanayokosa huduma ya maji yaondokane na kero hiyo.

Wanajeshi walalama kupokwa silaha, msaada wahitajika
Ahmed Ally: Banda atasubiri mwezi mzima