Mahirika matatu makubwa ya ndege (KLM,Qatar,na Ethiopia) yamejipanga kuongeza masafa zaidi ya ndege miezi mitatu baada ya maeneo mengine kufua anga .
Shirika la ndege la Ethiopia ambalo ndiyo shirika la kwanza la ndege kurejesha safari zake katika uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere , ambapo safari zitaongezeka kutoka mara nne kwa wiki na kufikia 14.
Mkurugenzi wa maendeleo uwanja wa ndege Kilimanjaro ,Catherine Mwakatobe amesema kuwa ,KLM imeongeza safari toka moja hadi nne , shirika la Qatari limeongeza ratiba ya safari zake kutoka tatu mpaka 12.
Ikiwa ni sehemu ya mwendelezo tangu kurejea kwa safari za ndege shirika la ndege la Rwanda litakuwa na safari tatu kwa wiki katika uwanja wa kimataifa wa Kilimanjaro .
Shirika la ndege la Uturuki limekuwa likifanya safari zake nyingi kutoka Instanbul kwenda KIA kabla ya mlipuko wa ugonjwa na Covid-19 na kusitishwa .
“Safari hizi za ndege zitatoa ujumbe mzito kwa dunia kuwa Tanzania hakuna virusi vya Corona,” alisema Mwakatobe .
Jana , ndege aina ya Dream-liner inayo milikiwa na shirika la ndege la Ethiopia ilitua uwanja wa kimataifa wa KIA ambapo wesafiri walipokelewa Mkuu wa mkoa wa mkoa huo Anna Mghwira na baadhi ya viongozi wa serikali. Tanzania ilikuwa nchi ya kwanza kufungua anga lake baada ya kufanikiwa kudhibiti.