Shirikisho la wakuu wa Polisi kwa nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO) wanatarajia kukutana Mei 24, 2017 jijini Arusha chini ya mwenyekiti wao wa sasa ambaye ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Ernest Mangu.
Hayo yamesemwa mapema hii leo Jijini Dar es salaam na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Advera Bulimba alipokuwa akizungumza na waandihshi wa habari,
Amesema kuwa mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba ambapo shirikisho hilo litajadili mambo malimbali ikiwemo jinsi ya kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka kwa kufanya operesheni za pamoja ili kukabiliana na makosa mbalimbali yakiwemo dawa za kulevya, wizi wa magari, usafirishaji haramu wa binadamu na ugaidi.
Aidha, katika mkutano huo utajadili utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa na Wakuu wa Upelelezi wa SARPCCO pamoja na kamati tendaji za sheria, Mafunzo na kamati tendaji ya Jinsia na watoto katika mkutano wao uliofanyika mwezi Machi mjini Bagamoyo.
Hata hivyo, Shirikisho hilo linaundwa na Nchi kumi na tano ambazo ni Tanzania, Angola, Botswana, Malawi, Lesoto, Mauritius, DRC, Msumbiji, Namibia, Afrika Kusini, Zambia, Zimbabwe, Swaziland, Madagascar na Syshelis.