Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto imesema kuwa itaendelea kuhamasisha Halmshauri zote nchini kununua viuadudu vya kibailojia kwa ajili ya kuua viluilui vya mbu waenezao Malaria vinavyotengenezwa na kiwanda cha Biotec product cha Kibaha.

Hayo yamesemwa leo Bungeni na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangala  wakati akijibu swali la Mbunge wa Gando Othman Omar Haji.

“Viuadudu hivi vimeanza kutengenezwa kuanzia mwezi Desemba 2016 na kwa sasa uhamasishaji huu unaendelea  na endapo viuadudu hivi vitatumiwa vizuri vitasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza kiwango cha maambukizi ya Malaria nchini”, Amesema Kigwangalla.

Aidha amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Ushirikiano na Serikali ya Cuba imeendelea kushirikiana katika mambo mengi ikiwemo pamoja na Sekta ya Afya tangu mwaka 1986 mkataba uliposainiwa kati ya Serikali hizi mbili.

Hata hivyo, ameongeza kuwa kupitia mkataba huo Serikali ya Tanzania imekuwa ikipokea madaktari bingwa kutoka Cuba ambao wamekuwa wakifanya kazi katika Hospitali za Muhimbili,Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya , Hospitali Tumbi na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma.

 

Trump aipa Tanzania mabilioni
Shirikisho la wakuu wa Polisi SADC kukutana jijini Arusha