Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amezitaka Hospitali zote za Halmashauri nchini kuwapima watoto wote wanaozaliwa katika Hospitali hizo ugonjwa wa Sikoseli, ili kujua hali zao mapema na kuwaanzishia matibabu.

Waziri Ummy ameyasema hayo wakati akizindua kampeni ya kuelimisha jamii juu ya Magonjwa Yasiyoambukiza yaliyofanyika katika Hospitali ya Sinza – Palestina, Jijini Dar es Salaam.

Amesema, “Waganga Wakuu wa Mikoa mkalisimamie hili nataka Hospitali zote za Halmashauri nchini ndani ya Miezi Sita zipime ugonjwa wa Sikoseli kwa watoto wanaozaliwa katika Hospitali hizo kabla sijashuka vituo vya Afya.”

Aidha, Ummy amesema zaidi ya asilimia 70 hadi 90 ya watoto wanaozaliwa na Sikoseli hupoteza maisha ndani ya kipindi cha Miaka Mitano ya mwanzo wa maisha yao kutokana na kutotambulika au kwa sababu ya unyanyapaa na kukosa elimu.

Maandamano: Viongozi wa Upinzani washambuliwa
Uteuzi mwingine wa Rais Samia, mabadiliko ya Uongozi