Serikali ya Nepal tayari imeanzisha jopo la kuchunguza sababu ya kutokea kwa ajali ya ndege Januari 15, 2023 iliyoanguka wakati ikikaribia kutua uwanjani, na ripoti hiyo inatarajiwa kutolewa ndani ya siku 45 zijazo.
Hayo yamesema na Waziri wa fedha wa Nepal Bishnu Paudel wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa juu ya uokozi unaendelea kufanywa na jeshi la nchi hiyo.
Ajali hiyo ndiyo mbaya zaidi tangu mwaka 2018, wakati ndege aina ya Dash 8 kutokea mjini Dhaka, Bangladesh kuanguka ilipokuwa ikitua mjini Kathmandu na kuwaua watu 51 kati ya abiria 71 walikuwemo.
Watu wasiopungua 309, wamekufa tangu mwaka 2000 katika ajali za ndege au helikopta nchini Nepal, taifa linalofahamika kwa kuwa na milima mirefu zaidi duniani ikiwemo Mlima Evarest.
Mwaka 2013, Umoja wa Ulaya ulikwishayapiga marufuku mashirika ya ndege ya Nepal kutumia anga ya kanda hiyo kutokana na wasiwasi juu ya usalama.