Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, David Silinde ametoa wiki mbili kwa Afisa Elimu Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu kukamilisha ujenzi wa vyoo vya wanafunzi katika shule mbili za msingi za Gidbiyo na Endahagichan pamoja na madarasa mawili na ofisi ya mwalimu ambazo hajikamilika zaidi ya miezi 11 kumi na moja tangu serikali itoe fedha kwa ajili ya ujenzi huo.
Ametoa maagizo hayo akiwa katika ziara ya siku moja katika wilaya ya Mbulu mkoa wa Manyara kukagua matumizi ya fedha milioni 47 na laki saba kwa kila shule zilizotolewa na serikali kupitia programu ya GPE LANES II kujenga madarasa na vyoo ambavyo wanafunzi walikuwa wanapata tabu kutokana na upungufu shuleni hapo.
Akiwa katika shule ya Msingi Endahagichan Naibu Waziri Silinde amemuagiza afisa elimu wa wilaya ya Mbulu Fatma Msangi kuhakikisha ujenzi wa vyoo na madarasa katika shule hizo unakamilika ndani ya wiki na kupelekewa taarifa ofisini kwake mala moja.
Kwa upande wake Afisa elimu wa halmashauli ya wilaya ya Mbulu Fatma Msangi amemueleza Naibu waziri Silinde kuwa hatua atakazochukua kwasasa ni kuwashusha vyeo mratibu wa elimu Slaqwara Nade na walimu wakuu wawili Ezekiel Kunsel pamoja na Ladislaus Blazi ambao wameshindwa kusimamia kukamilisha kwa ujenzi huo kwa wakati.
Hata hivyo Naibu waziri Silinde amezungumza na mwananchi wa kijiji cha Endahagichan Marsel Arusha pamoja na fundi wa ujenzi wa choo amba wamesema kuwa wananchi wa kijiji hicho wlijitoa kwa kubeba mawe, kuchimba shimo la choo, kuchanganya kokoto ila tatizo kubwa lililochelewa kukamilika kwa wakati ni ubovu wa barabara hasa wakati wa masika.