Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mwita Waitara, amezitaka taasisi za Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Shirika la Wakala wa Meli (TASAC) na Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) kufanya tathmini ya kina kabla ya kuanza matengenezo ya meli ya MV Mbeya II.

Rais Mwinyi asema chanjo ya corona ni hiari

Waitara ametoa kauli hiyo baada ya kukagua miundombinu katika bandari za Kiwira na Itungi wilayani Kyela na kubaini ucheleweshaji wa matengenezo ya meli hiyo iliyosimama kutoa huduma katika Ziwa Nyasa mapema mwezi Aprili kutokana na hitilafu za kifundi.

“Meli hii imesimama zaidi ya wiki tatu sasa na ninajua meli hii bado iko kwenye muda wa uangalizi hivyo ninawaagiza TPA, TASAC, DMI na Kampuni ya Songoro kukaa na kuwasilisha ripoti haraka iwezekaavyo ili matengenezo yaanze” ameagiza Naibu Waziri Waitara.

Aidha, Naibu Waziri Waitara imeitaka Kampuni ya Songoro Marine kufanya tathmini ya Chelezo ambayo imekuwa bandarini Kiwira kwa zaidi ya mwaka bila kufanyiwa matengenezo ili kujiridhisha na ufanisi wake kabla ya kupandisha meli zinazohitaji matengenezo.

Uhamiaji yalaani kitendo kilichofanywa na Askari wake, yawasimamisha kazi
Silinde atoa wiki mbili kwa Afisa Elimu Mbulu