Idara ya Uhamiaji nchini imelaani kitendo kilichofanywa na askari wake, ambaye alitumia nguvu dhidi ya Alex Kyai, katika ofisi ya Uhamiaji Kurasini jijini Dar es Salaam.

Taarifa hiyo iliyotolewa leo Mei 30, 2021 na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makala, imeeleza, “Napenda kutumia fursa hii kutoa taarifa kwa umma kuhusu tukio la askari wa Uhamiaji kutumia nguvu dhidi ya Ndugu Alex Raphael Kyai kama ilivyoonekana katika video fupi iliyosambaa katika mitandao ya kijamii.”

“Idara ya Uhamiaji inakiri kutokea kwa tukio hilo na pia inaalani kitendo kilichofanywa na askari wa Uhamiaji kwa kutumia nguvu,” ameeleza Dkt. Makakala.

Tayari Idara ya uhamiaji imewasimamisha kazi askari wake watatu waliohusika katika tukio hilo kama ilivyoonekana katika video fupi iliyosambaa.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kulaghai na kupokea fedha kutoka kwa Wateja mbalimbali ili waweze kupata pasipoti kwa haraka pia amekuwa akijitambulisha kama Mtumishi wa Taasisi nyeti ikiwemo TAKUKURU.

“Hatua ambazo Idara imechukua dhidi ya Askari, tumewasimamisha kazi kupisha uchunguzi wa tukio lenyewe lakini pia Mtuhumiwa tumemfikisha kwenye mamlaka husika ili aweze kuendelea na utaratibu mwingine kisheria,” amesema Dkt. Makakala.

Watakaochomwa chanjo ya Corona kupewa donge nono
Maagizo ya Waitara kwa TPA, TASAC