Wawakilishi wa Tanzania na Afrika Mashariki na Kati ‘CECAFA’ ‘Simba Queens’ watacheza Nusu Fainali ya Pili ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Mabingwa watetezi Mamelodi Sundowns.

Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, imemaliza kinara wa Kundi B wakifikisha alama 9, ikishinda michezo mitatu ya hatua hiyo, na kikanuni itakutana na Mshindi wa Pili wa Kundi A ambaye ni Simba Queens.

Simba Queens iliyomaliza nafasi ya pili katika msimamo wa Kundi A baada ya kuibamiza Green Buffalo juzi Jumamosi (Novemba 05), itacheza mchezo huo wa Nusu Fainali keshokutwa Jumatano (Novemba 09), katika Uwanja wa Moulay Hassan mjini Rabat.

Mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali utashuhudua wenyeji AS FAR wakicheza dhidi ya Bayelsa Queens ya Nigeria iliyomaliza nafasi ya pili kwenye msimamo wa Kundi B.

Michuano hiyo itafikia tamati Jumapili (Novemba 13) kwa washindi wa michezo ya Nusu Fainali kukutana kwenye mchezo wa Fainali, utakaopigwa katika Uwanja wa Prince Moulay Abdellah uliopo mjini Rabat.

Timu zitakazopoteza katika Hatua ya Nusu Fainali zitacheza mchezo wa kumsaka mshindi wa tatu na wa nne Jumamosi (Novemba 12), katika Uwanja wa Prince Moulay Abdellah uliopo mjini Rabat.

Katibu Mkuu akataa uongozi wa kurudi nyuma
Ajali ya ndege Bukoba: Safari za anga zasitishwa