Kikosi cha Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC leo Alhamis (Desemba 16), kinaondoka jijini Dar es salaam kuelekea Bukoba mkoani Kagera.
Simba SC itacheza dhidi ya Kagera Sugar keshokutwa Jumamosi (Desemba 18), katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba saa kumi jioni.
Mabingwa hao wanaondoka jijini Dar es salaam, baada ya kushinda mchezo wa mzunguuko wa tatu wa Kombe la Shirikisho dhidi ya JKT Tanzania juzi Jumanne (Desemba 14), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.
Mchezo uliopita wa Ligi Kuu Simba SC ilikutana na Young Africans Uwanja wa Benjamin Mkapa na kuambulia sare ya bila kufungana.
Simba SC inashika nafasi ya pili kwenye Msimamo wa Ligi Kuu kwa kuwa na alama 18, ikiongozwa na YoungA fricans iliyofikisha alama 20, huku Kagera Sugar ikiwa nafasi ya tisa ikiwa na alama 9.