Klabu ya Simba SC itaandika historia Barani Afrika na Tanzania kwa kuwa miongoni mwa Klabu 24 zitakazoshiriki mara ya kwanza Michuano ya CAF SUPER LEAGUE barani huo.
Michuano hiyo imezinduliwa rasmi leo Jumatano (Agosti 10) mjini Arusha katika Mkutano Mkuu wa kawaida wa 44 wa Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’.
Klabu 24 kutoka mataifa 16 zitashiriki michuano hiyo, kulingana na viwango vya ubora upande wa vilabu ambavyo vinatambuliwa na ‘CAF’.
Orodha ya vilabu vitakavyoshiriki michuano hiyo ni Al Ahly, Zamalek, Pyramid, Al Masry, Wydad AC, Raja Athletic, RS Berkane, Esperance, Etoil Sportive Du Suhel na Orlando Pirates.
Nyingine ni Kaizer Chiefs, Mamelodi Sundowns, JS Kabyile, CR Belouzidad, E.S Setif, TP Mazembe, Horoya AC, SC Enyimba, Petro de Luanda, Simba SC, Asante Kotoko, Al Hilal, Asec Mimosas na Coton Sport.
Bingwa wa michuano hiyo atavuna zaidi ya bilioni 233 za Tanzania
Utaratibu rasmi wa michuano hiyo utatangazwa na CAF hivi karibuni.