Idara ya Habari na Mawasilino ya Simba SC imetoa ufafanuzi wa alipo Kocha Msaidizi Juma Ramadhan Mgunda, baada ya kutoonekana katika Uwanja wa mazoezi ‘Mo Simba Arena’.

Kocha Mgunda alikiongoza Kikosi cha Simba SC kwenye maandalizi na Mchezo wa Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ Hatua ya 32 Bora dhidi ya Coastal Union iliyokubali kufungwa 1-0, Uwanja wa Benjamin Mkapa Jumamosi (Januari 27).

Meneja wa Habari na Mawasilino Ahmed Ally amesema kutoonekana kwa Kocha Mgunda katika mazoezi ya kikosi chao jana Jumatano (Februari Mosi), kumesababishwa na changamoto binafsi.

Amesema Kocha huyo amelazimika kurejea jijini Tanga, na atakapomaliza changamoto hizo, atajiunga na timu na kuendelea kusaidiana na Kocha Mkuu Roberto Oliviera ‘Robertinho’, ambaye tayari amesharejea nchini na kuanza kazi mara moja.

“Watu hawapasi kujiuliza aliko kocha wetu msaidizi Juma Mgunda. Taarifa rasmi ni kwamba Mgunda anauguliwa na mama yake mzazi, hivyo ameenda kwao Tanga mara moja kumuuguza na hali yake ikiwa vizuri atarudi kuungana na timu.”

“Mama yake anaumwa muda mrefu na asingeweza kuondoka kuiacha timu, hivyo urejeo wa Robentinho unampa nafasi Mgunda kurudi Tanga kwa ajili ya mama yake” amesema Ahmed Ally

Kikosi cha Simba SC kinaendelea na maandalizi ya mchezo wa Mzunguuko wa 22 wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Singida Big Stars, utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa kesho Ijumaa (Februari 03).

Young Africans yaijibu SportPesa, hatujakurupuka
Dkt. Mpango, Chiwenga wajadili ushirikiano