Mabosi wa klabu ya Simba SC wameamua kujilipua kwa kutuma maombi Bodi ya Ligi (TPLB) ili kucheza mechi yao na Coastal Union.

Mechi hiyo katika ratiba iliyotolewa na TPLB, haikupangiwa tarehe licha ya kuonekana itakuwa ni Septemba 16 kutokana na muingiliano na mechi za kimataifa za timu ya taifa, hivyo mabosi wa Simba wameona isiwe tabu kwa kutaka ipigwe kabisa kwa kuhofia kukaa mwezi mzima bila kucheza mechi.

Kwa mujibu wa ratiba, Simba SC itarudi uwanjani katika mechi za raundi ya nne kati ya Oktoba 3 na 4 kwa kusafiri hadi Mbeya kuvaana na Tanzania Prisons, hivyo wanaona ni vyema wacheze kabisa mechi hiyo dhidi ya Wagosi ambayo haijapangiwa tarehe kama ilivyo kwa zile za Young Africans Vs Namungo FC, Azam FC Vs Singida Fountainm Gate zitakazochezwa jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, timu hizo nazo zitakuwa na mechi nyingine raundi ya nne ndani ya September ni Coastal Union watakaocheza na Tabora United, Namungo na Mashujaa FC.

Azam FC na Young Africans pia baada ya kucheza raundi mbili itacheza mechi zake nyingine za Ligi Kuu, Oktoba mwaka huu.

Azam FC itakuwa ugenini Oktoba 3 kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma kuivaa Dodoma Jiji, Ihefu FC itaikaribisha Young Africans ndani ya Uwanja wa Highland Estate, wilayani Mbarali mechi hiyo itachezwa Oktoba 4 mwaka huu.

Simba SC kwa kutotaka kuwa na kiporo imeomba mechi hiyo dhidi ya Coastal ipigwe kabisa Septemba na tayari wametuma ombi kwa Bodi na kama litakataliwa basi mechi hiyo itachezwa na za wenzao Young Africans na Azam FC mapema Oktoba.

Habari za ndani ya klabu hiyo zinasema mabosi wamekubaliana na kocha kutokuwa na viporo kwani wakati mwingine huwa vinachosha wachezaji.

KKKT inafanya kazi kwa ukaribu na BAKWATA - Injinia Kitundu
Neymar kusubiri hadi Septemba