Tetesi za aliyewahi kuwa kocha mkuu wa Young Africans Mwinyi Zahera ‘PAPA ZAHERA’ za kutua kwa mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba SC kama Mkurugenzi wa Ufundi, zimekanushwa na uongozi wa klabu hiyo.


Tetezi kuhusu Zahera ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Ufundi wa Gwambina FC, zilianza kuchukua nafasi kwenye mitandao ya kijamii jana Jumapili (Januari 24), saa chache kabla ya kutambulishwa kwa kocha mkuu mpya wa Simba SC Didier Gomes Da Rosa.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amesema hawana mpango wa kumpa kazi Zahera, na taarifa za kuhusishwa na mpango wa kumuajiri Mcongoman huyo kama Mkurugenzi wa Ufundi wanaziona zikisambaa kwa kasi, kupitia mitandaio ya kijamii.


“Kuhusu huyo Zahera mimi simjui na tayari tumeshatangaza benchi letu la ufundi ikiwa ni pamoja na kocha mkuu na kocha wa makipa, ipo nafasi nyingine ambayo tutaitangaza hivi karibuni.” Amesema Barbara.

Simba SC imemtambulisha Milton Nienov raia wa Brazil kuwa kocha wa makipa na Didier Gomes raia wa Ufarasa kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo inayoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika, ikiwa hatua ya makundi na Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho wakiwa ni mabingwa watetezi.

Mtanzania awa Mwafrika wa kwanza kushinda tuzo utafiti wa miamba
Afisa wa ngazi ya juu Korea Kaskazini akimbilia Korea Kusini