Klabu ya Simba SC imetuma mashushushu nchini Guinea kwa ajili ya kuandaa mazingira ya kufikia na kuwachunguza wapinzani wao Horoya AC.
Simba SC Februari 11 itacheza mchezo wake wa kwanza wa Kundi C ugenini dhidi ya Horoya AC katika Uwanja wa General Lansana Conté uliopo mjini Conakry.
Taarifa kutoka Simba SC zinaeleza kuwa, tayari mashushushu hao wameshawasili mjini Conakry na kuanza taratibu zote, ambazo zitawezesha wachezaji na baadhi ya viongozi watakaoambatana na timu kuishi kwa usalama wakati wote watakapokuwa huko.
“Kuna baashi ya viongozi wa Simba SC tayari wameshafika nchini Guinea ikiwa ni mapema kabisa kwa ajili ya kuangalia utaratibu wa wapi timu itafikia pamoja na sehemu nzuri ya kufanyia mazoezi.”
“Ukiachana na hilo pia wamekwenda kuangalia hali ilivyo kwa sasa nchini humo, na kuwachunguza wapinzani wetu ambao pia kuna mtaalamu wa kusoma michezo miwili ya wapinzani, ambayo wacheza kabla ya kukutana na Simba SC mapema mwezi Februari.” kimeeleza chanzo cha habari kutoka Simba SC
Timu nyingine zilizopangwa katika Kundi D ni Raja Casablanca ambayo itaanzia nyumbani mjini Casablanca kwa kuikabili Vipers SC ya Uganda.