Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahme Ally amethibitisha kurejea kambini kwa kikosi chao, tayari kwa maandalizi ya mchezo wa Mzunguuko watatu wa Kundi B, Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Wydad Casablanca, Jumamosi (Desemba 09).

Simba SC itacheza ugenini nchini Morocco, ikiwa na lengo la kusaka ushindi ili kufufua matumaini ya kuwa moja ya timu mbili zitakazofuzu hatua ya Robo Fainali kupitia Kundi B.

Ahmed Ally ametumia Kurasa zake za Mitandao ya Kijamii kuthibitisha kurejea kambini kwa kikosi cha Simba SC, ambacho kilipewa mapumziko ya siku moja, baada ya kurejea Dar es salaam kikitokea Botswana.

Ahmed Ally ameandika: Kikosi kinarejea kambini hii leo kuanza maandalizi ya mchezo wetu dhidi ya Wydad Casablanca December 9.

Wydad imepoteza mechi mbili za mwanzo lakini hiii haitupi nafasi ya kwenda kichwa kichwa kwani Wydad ni sawa na Mnyama mkali aliyesinzia huwezi jua ataamka saa ngapi na ataamkia kwa nani?!!

Sisi tunapaswa kujiandaa tukiamini tunakwenda kucheza na mpinzani mgumu tukimkuta bado amelala fresh tunapita nae tukimkuta ameamka tunakomaa nae.

Simba SC yamaliza dakika 540 kimataifa
Young Africans haijakata tamaa Afrika