Uongozi wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Young Africans umeweka wazi licha ya sare ambayo waliipata dhidi ya Al Ahly lakini bado wanajiona bado wana nafasi ya kusonga mbele kwenye Kundi lao na kutinga hatua ya Robo Fainali.

Young Africans katika mchezo wa juzi Jumamosi (Desemba 02) walilazimishwa sare ya bao 1-1 katika mchezo wa Mzunguuko wa Pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly uliofanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Makamu wa Rais wa Young Africans, Arafat Haji amesema kuwa: “Licha ya kutoka sare katika mchezo huu tunayo kila sababu ya kupambana kwa ajili ya kuhakikisha kuwa tunaivuka hatua hii na kutinga hatua inayofuata ya michuano hii.

“Al Ahly hakuna ambaye hafahamu kuwa ni timu kubwa Afrika lakini ni bingwa mtetezi wa hii michuano mikubwa, baada ya hii sare tunatakiwa kuhakikisha kuwa tunafanya vizuri katika michezo yetu ijayo ili tusitoke zaidi katika malengo yetu.

“Katika kuhakikisha kuwa tunakuwa bora zaidi lazima tukubaliane na ukweli, tutachukuwa maoni na tutarudi tukiwa imara zaidi kikiubwa ni kufikia malengo yetu na tunawashukuru sana mashabiki wa Young Africans kwa sapoti yao kwetu,”amesema Arafat.

Simba SC yarejea kambini kuiwinda Wydad
Idadi waliofariki kwa mafuriko Hanang' yafikia 49