Idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na mafuriko yaliyotokea wilayani Hanang’ mkoa wa Manyara imeongezeka na kufikia watu 49 baada ya kupatikana kwa miili mingine miwili.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga hii leo Novemba 4, 2023 amesema idadi ya majeruhi bado ni 85.

Aidha amesema kuwa shule za msingi za Katesh na Dumanang zitatmika kuhifadhi waathirika wa mafuriko hayo.

Sendiga pia amewataka Wananchi kuhama mara moja maeneo ya hatari, ili kuepukana na madhara mengine yanayoweza kutokea.

Young Africans haijakata tamaa Afrika
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Desemba 4, 2023