Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limesema litawakamata na kuwachukulia hatua kali za kisheria baadhi ya wamiliki wa vyombo vya moto, wanaotumia kigezo cha mwisho wa mwaka kuingiza vyombo vyao ambavyo vinachangamoto za kiufundi kusafirisha abiria maeneo mbalimbali hapa nchini.

Hayo yamesemwa mapema na Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Zauda Mohamed katika kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani na nchi Jirani huku akibanisha kuwa kumekuwepo na tabia ya baadhi ya wamiliki kutumia kigezo cha wingi wa abiria na mwisho wa mwaka kuingiza magari mabovu barabarani.

Amesema, Jeshi la Polisi kupitia kikosi cha usalama Barabarani Mkoani humo hakitowafumbia macho wamiliki watakao bainika kuingiza magari mabovu barabarani huku akisema kikosi hicho kitaendelea kufanya ukaguzi wa vyombo vya moto mara kwa mara na kutoa elimu kwa madereva na abiria wanaotumia vyombo hivyo.

Aidha amewataka madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kumaliza kabisa ajali ambazo zimekuwa zikisababisha ulemavu na kuwaacha wananchi wakiwa na ulemavu wakudumu ambapo amewataka madereva ambao wamekuwa wakiendesha umbali mfupi kuwatumia madereva wazoefu kuwaendesha kama wanakwenda safari ndefu.

Sambamba na hilo ametoa wito kwa wazazi wanaotumia kipindi hiki cha mwisho wa mwaka kuwasafirisha watoto wadogo Kwenda kuwasalimia ndugu na jamaa maeneo tofauti tofauti, kuhakikisha watoto hao wanakuwa na uangalizi wa karibu ili kupunguza vitendo vya upoteaju wa Watoto .

Kwa upande wake mmoja wa wasafiri Mchungaji Getruda Kyando pamoja na kuliomba Jeshi hilo kufanya ukaguzi wa mara kwa mara piq amekipongeza kikosi hicho kwa kutoa elimu na mawasiliano ya moja kwa moja kwa abiria ambayo yatasaidia kutoa taarifa kwa wakati pindi madereva wanapokiuka sheria za usalama Barabarani.

Nao baadhi ya madereva wanaofanya safari zao ndani na nje ya nchi wamesema kumekuwepo na ongezeko la magari kipindi hiki cha mwisho wa mwaka huku wakiwataka madereva wenzao wasiofuata sheria za usalama barabarani kuhakikisha wanafuta sheria hizo ili kupunguza ajali hapa nchini.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Desemba 4, 2023
Mafuriko Hanang vifo vyafikia 20