Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga amesema Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Mkoani humo, zimesababisha madhara ambapo alfajiri  ya leo Watu watano wamefariki na  na wengine zaidi ya 10 wamejeruhiwa.

Amesema Nyumba kadhaa zimezingirwa na maji kutokana na mafuriko hayo na zingine zimeharibiwa huku timu ya uokozi ikiwa eneo la tukio kwa ajili ya kutoa msaada na kuwatafuta manusura kwani baadhi ya watu hawajulikani walipo.

Kufuatia adha hiyo ya mafuriko, shughuli za kawaida kiuchumi zimetatizika na baadhi ya barabara hazipitiki hivyo kuleta changamoto ya usafiri kwa Wananchi wa eneo hilo na maeneo jirani.

Endelea Kufuatilia Dar24 Media kwa taarifa zaidi

Mafuriko Hanang vifo vyafikia 20
Silaa: Hakuna huruma wanaovunja sheria kipindi cha Uchaguzi