Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limetoa tahadhari kwa mashabiki wa klabu za Simba SC na Young Africans, kuelekea mchezo wa kesho Jumamosi (Julai 03).
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Muliro Jumanne amesema, yeyote ambae ataingia uwanjani kwenye mchezo huo utakaochezwa kwenye wa Benjamin Mkapa hatakiwi kwenda na silaha kama bunduki, kisu, panga au jiwe lakini pia chupa za aina yoyote zimepigwa marufuku.
Kamanda Muliro pia amesema: “Pasipokua na sababu ya lazima watoto wadogo wasiende uwanjani, pia magari yote yatakayoruhusiwa ni yale yenye vibali maalum na yataelekezwa maeneo ya kupangwa”
Simba SC yenye alama 73 katika msimamo wa Ligi Kuu, itakuwa mwenyeji kwenye mchezo huo, ambao umepangwa kuanza saa 11 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.