Hatimaye kiungo fundi wa mpira wa Young Africans, Haruna Niyonzima amevunja ukimya baada ya sintofahamu iliyojitokeza kuelekea mchezo wao wa kesho Jumamosi (Julai 03) dhidi ya Simba SC.

Niyonzima amesema anashindwa kuelewa utovu wa nidhamu aliouonyesha kambini, kwani alikuwa anaumwa na kusababisha kukosekana katika safari ya mchezo wa nusu fainali kombe la Shirikisho (ASFC) dhidi ya Biashara United mkoani Tabora.

“Nilikuwa ninaumwa na dozi yangu ya dawa ilimalizika Jumatatu, siku iliyofuata nilikuwa niingie kambini, lakini wakati najiandaa kwenda nilipata ujumbe kwamba sitakiwi kwenda na sasa sitakuwepo kwenye mipango ya mchezo wa keshi Jumamosi dhidi ya Simba SC.

Niyonzima na Lamine Moro waliripotiwa kufukuzwa kambini Avic Town Kigamboni jijini Dar es salaam kwa utovu wa nidhamu.

Metacha hataki 'MASKHARA'
Simba SC, Young Africans zaonywa