Klabu ya Simba leo imewapa raha ya aina yake mashabiki wake nchini kwa kufanikiwa kupiga hatua kubwa katika mashindano ya Kombe la Klabu Bingwa Barani Afrika, baada ya kuizamisha Nkana FC ya Zambia.

Hatua hiyo inaweza kuturudisha kwenye kumbukizi ya maneno ya Rais wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete aliyewahi kukisihi kikosi cha timu ya Taifa, “nipeni raha.” Leo, raha ya soka aliyoitaja Dkt. Kikwete inadhihirika wazi kwenye nyuso za mashabiki wa Simba.

Simba imefanya kazi nzito ya kuking’oa kisiki hicho kutoka Zambia kwa kugawa kichapo cha 3-1 (Kwa ujumla magoli 4-3), goli la mwisho na la ushindi likipachikwa kimyani na Mzambia Clatous Chama katika dakika ya 88.

Matokeo hayo yameweka historia ya timu hiyo ya Msimbazi kutinga kwa mara ya kwanza katika hatua ya makundi kwenye kombe hilo baada ya miaka 15. Mara ya mwisho ilikuwa mwaka 2003.

Mohammed Dewji ametamba kwa kuweka picha akiwa anapiga push up kuonesha ubabe wa timu hiyo, na ameeleza kuwa lengo lao ni kuwa Mabingwa wa Afrika.

“Alhamdulillah. Hongereni Simba. Narudia tena: Lengo letu ni kuwa Mabingwa wa Afrika,” ameandika.

Mo ambaye ni muwekezaji mkuu katika timu hiyo, anaendelea kupata sababu za kuhakikisha anatimiza ndoto ya kujenga uwanja wa kisasa wa timu hiyo kwani itaanza kushiriki mitanange mizito barani Afrika endapo ndoto yao itatimia mwaka huu ya kuwa mabingwa wa Kombe la Klabu Bingwa Barani Afrika.

 

View this post on Instagram

 

Alhamdulillah ?? Hongereni Simba, Narudia tena: Lengo letu ni kuwa Mabingwa wa Afrika!

A post shared by Mohammed Dewji (@moodewji) on

Nkana walikuwa wa kwanza kuifunga Simba, lakini hadi kipindi cha kwanza kinamalizika tayari matokeo yalikuwa 2-1; na Simba ilitegua kitendawili cha kuelekea kwenye matuta kwa kupachika goli lingine.

Maandamano kupinga ugumu wa maisha yasababisha vifo
Rais Magufuli awatangazia hatari watendaji 100 wa Serikali, wapo mawaziri na wabunge