Uongozi wa Klabu ya Singida Fountan Gate, umeweka mikakati kabambe ya kuiwezesha timu yao kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Singida Fountain Gate FC inatarajia kushuka dimbani kesho ljumaa katika mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya JKU ya Zanzibar katika mtanange utakaopigwa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar es salaam, Mtendaji Mkuu wa Singida Fountain Gate FC, Sikwane Olebile, amesema timu imefanya maandalizi ya kutosha na kuhakikisha inafanya vizuri katika mechi ya awali na zitakazofuatia.
Olebile amesema klabu imeiandaa timu na inaendelea kuiandaa kikamilifu katika Nyanja zote na kuhakikisha inafanya vizuri.
Alisema timu inasimamivwa kwa karibu na uongozi na kuiwezesha kupata mahitaji yote muhimu.
Tunashiriki kwa mara ya kwanza mashindano haya hivyo ni lazima tujipange vizuri, hatutaki timu ifanye vibaya na kuondolewa katika hatua za awali” amesema.
Mtendaji huyo amesema katika mchezo dhidi ya JKU, mashabiki wataingia dimbani bure na kuwataka mashabiki wa soka kujitokeza kwa wingi. Iwapo Singida Fountain Gate itaiondoa katika mashindano jKU, itacheza hatua itakayofuata dhidi ya timu ya Future ya nchini Misri.