Ikiwa kwenye mpango wa kuweka kambi nchini Tunisia kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2023/24, Klabu ya Singida Fountain Gate FC imeanza kutambia usajili wake.

Timu hiyo imekamilisha mpango wa kuwaongezea mikataba baadhi ya wachezaji wake iliokuwa nao msimu wa 2022/23, ikiwa ni Bruno Gomes mwenye mabao 10, Yusuph Kagoma na Aziz Andambwile.

Afisa Habari wa Singida Fountain, Hussein Massanza amesema kuwa wanatambua kuwa ushindani ni mkubwa hivyo usajili wao utakuwa wenye malengo makubwa.

“Malengo makubwa kwenye usajili wetu ni kuwa na timu imara ambayo itakuwa na ushindani jambo ambalo linatufanya tuwe makini kwenye kuwaongezea mikataba wachezaji pamoja na kuwa na kikosi imara.

“Kila mmoja anatambua kuwa tunashiriki mashindano ya kimataifa, ambacho tunakifanya ni kuongeza nguvu kwenye kila idara hivyo mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi.” amesema Massanza.

Usitumie Dawa bila kupima ni hatari - Dkt. Faustine
Try Again atema cheche za usajili 2023/24