Zaidi ya wafanyakazi 1000 wa kiwanda cha nguo cha Winds Group ltd (Mazava) kilichopo mkoani Morogoro wamejikuta katika sintofahamu baada ya kuzuiwa kuingia kiwandani hapo leo.
Hayo yamejiri baada ya uongozi wa kiwanda hicho kutangaza kuwapa likizo ya miezi 3 wafanyakazi wake bila malipo.
Imedaiwa kuwa wafanyakazi hao walitangaziwa kuhusu likizo hiyo lakini hawakukubali na wameenda kiwandani hapo ili kujua hatima yao kwa miezi hiyo ambayo watakuwa nyumbani.
Kwamujibu wa wafanyakazi hao kiwanda kilitakiwa kufungwa Mei 24 lakini hali imekuwa tofauti na wafanyakazi wamezuiwa kuingia kiwandani kuendelea na shughuli kuanzia leo, Mei 15.
Mazava ni moja kati ya kiwanda kilichoajiri watu wengi Mkoani Morogoro, kikiwa na zaidi ya watu 1,000