Wizara ya Afya Zanzibar imepokea mashine moja ya kupima Corona kati ya tatu zilizokuwa zimeagizwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Mashine hiyo iliyowasili inatoka Korea Kusini na inauwezo wa kutoa majibu ndani ya masaa manne kwa vipimo vya watu 96 hivyo inauwezo wa kutoa majibu ya vipimo 288 kwa siku.

Kuwasili kwa mashine hii ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein alilolitoa Machi 25, alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa maabara ya uchunguzi katika kijiji cha Bungi wilaya ya Kati Unguja.

Mashine mbili zilizobaki zinatarajiwa kuwasili wakati wowote kutoka hivi sasa na zinatarajiwa kufungwa Unguja na Pemba.

Watoto 100 washambulishwa na ugonjwa unaohusishwa na Corona
Sintofahamu ya wafanyakazi kiwanda cha Mazava, likizo miezi 3 bila malipo