Maana halisi ya neno Kabila ni jamii ya binadamu yenye umoja fulani upande wa lugha na utamaduni wa maisha yao ya kila siku na makabila haya yanaweza kugawanyika kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo hali ya kijiografia, maeneo, lugha na hata maumbile bila kusahau mila na desturi.

Kuna kabila moja la jamii ya Wambilikimo linaloaminiwa kuwa ni la asili linaloishi kwenye ukanda wa katikati mwa bara la Afrika, hawa ni watu wafupi wakifahamika kwa jina jingine kama Nigrillo na kwa wastani watu wazima wa kabila hilo wana urefu wa mita 1.3 hadi 1.4.

Wambilikimo ni binadamu wa makabila ambayo miili yao ni mifupi kuliko kawaida. Wataalamu wanatumia jina la Kiingereza lenye asili ya Kigiriki la ‘Pigmy’ kwa wasiofikia sm 150 na ‘pygmoid’ kwa waliozidi kidogo kipimo hicho na Watu wa aina hiyo wa kwanza kufikiriwa ni wale wa Afrika ya Kati, ambao ni Waaka, WaefĂ© na Wambuti.

Pia wapo Wambilikimo wa Watwa wa Rwanda na Burundi na kama kipimo kinachotumika ni sm. 155, basi kuna makabila ya namna hiyo hata nchini Australia, Thailand, Malaysia, visiwa vya Andamani (India), Indonesia, Ufilipino, Papua New Guinea, Bolivia, Brazil na Asia Kusini-mashariki.

Mbilikimo wapo wa aina mbili, mbilikimo wa asili (pygmy), na mbilikimo wa ugonjwa (dwarf), Wale wa nchini Kongo ni mbilikiko wa asili kwani maumbile yao ni ya asili na yanatokana na mazingira yao ya asili na umbilikimo wa aina hii ni wa huzaliwa na mbilikimo, yaani kizazi chao ni cha namna hiyo.

Kuna mbilikimo wa aina nyingine ambao wanapata matatizo ya mwili kushindwa kutengeneza ‘hormones’ zinazohitajika ili mwili kukua, na hivyo kubaki na umbo la kitoto maisha yao yote; hawa wanajulikana kama dwarfs. Mbilikimo wa aina hii huweza kutokea katika familia yoyote ile, wazazi wawili warefu wanaweza kuzaa mbilikimo wa aina ya dwarf.

Theories zinazonyesha kuwa, ‘evolutionary process’ iliyosababisha waafrika wakawa na ngozi nyeusi kutokana na mazingira ya joto la tropical, ndiyo pia iliyosababisha watu waliokuwa wakiishi kwenye misitu mizito kama vile Kongo kuwa wafupi kwa vile miili yao ilikuwa inakosa mwanga wa jua kutengeneza vitamin D.

Hivyo, miili yao ikawa haiwezi ku- ‘absrob calcium’ ya kutosha jambo liliosababisha wawe na mifupa midogo na hivyo kuwa na miili midogo. Misitu ya Kongo ndiyo yenye mbilikimo wengi wa aina hiyo ikifuatiwa na misitu ya Amazon huko Brazili na sehemu nyingine za dunia kama Papua New Guinea na Australia ambako pia kuna mbilikimo wanaoishi katika Misitu mikubwa.

Kwa mujibu wa utafiti wa kianthropolojia, umethibitisha kwamba watu wa kabila la mbilikimo ni warithi wa ustaarabu wa Sangha uliokuwepo kabla ya historia ya binadamu na ingawa Wabilikimo ni wafupi, lakini wana nguvu kubwa na wote ni wawindaji hodari na hujiita “watoto wa misitu”.

Wambilikimo ni wakazi asili wa kanda ya Afrika mashariki na kati, hadi sasa bado wanaishi kwenye maeneo ya misituni katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, Jamhuri ya Kongo, Afrika ya Kati, Burundi, Rwanda, Uganda na kabila jingine la Batwa ni wenyeji wa misitu mikubwa ya Ikweta katika eneo zima la Afrika ya kati.

Zamani watu wa kabila la mbilikimo walipenda kujifunika mwili kwa majani ya mtende, na kujipamba kwa mifupa ya tembo, pembe za mbuzi na magamba ya kobe, lakini kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watalii wanaotembelea vijiji vyao, wameanza kujifunza kuvaa nguo, lakini nguo zao zote walipewa na watalii.

Mbilikimo wanawake wanajua kutengeneza vipodozi vya asili kwa kuchanganya juisi ya matunda yenye rangi mbalimbali na maziwa ya mama, na kuchora michoro ya mapambo usoni, ili kurembesha nyuso zao na pia wanasema urembo huo huwakinga na mashetani.

Jamii ya watu Mbilikimo eneo la Asia Kusini-Mashariki.

Mbilikimo wanaume wote ni wawindaji hodari, wanatumia upinde waliotengeneza wenyewe kuwinda wanyama wakubwa kama tembo na wanapenda sana kula mchwa wakiamini kuwa inasaidia kujenga afya na pia hutunza sana misitu wanayoitegemea kimaisha, wakiruhusiwa kukata miti iliyokauka tu, kwa ajili ya kupata kuni za kupikia.

Inasemekana kulikuwahi kutokea timu moja ya wachunguzi iliyofika kwenye vijiji wanavyoishi mbilikimo, timu hiyo ilikata ovyo matawi ya miti, kitendo ambacho kiliwakasirisha wanavijiji wa eneo hilo na kupelekea timu hiyo kufukuzwa mahala hapo.

Hawa Mbilikimo kundi la watu wenye desturi za kipekee barani Afrika, lakini hivi sasa kabila la mbilikimo liko hatarini kutokweka na waliobaki kwa wingi ni wale wa aina ya Bayaka wanaopatikana nchini Cameroon, likiwa na watu wasiozidi elfu 40.

Makabila mengine mawili yanayofuata kwa ukubwa yana watu 3,700 na 1000 na Serikali ya Cameroon inachukua hatua katika kuhifadhi kabila la mbilikimo linalokabiliwa na hatari ya kutoweka na mbali ya juhudi zinazofanywa na serikali hiyo, masuala ya kuboresha maisha yao, pia yamefuatiliwa na mashirika ya kimataifa.

Lakini pia, baadhi ya nchi zimetekeleza sera maalumu kwa mbilikimo wanaoishi katika nchi hizo, zikiwahamasisha waondoke misituni na kuishi kama watu wa kawaida. Kutokana na kuongezeka kwa mawasiliano na jamii ya nje, lakini hata ustaarabu wa kisasa umeleta mabadiliko kwa kabila hilo, na wameanza kuvaa nguo na kutumia vitu vya kisasa kama vile sabuni, mafuta nk.

Ingawa hali iko hivyo, watu wengi wa kabila la mbilikimo bado wanapendelea kuishi maisha ya jadi misituni na katika uchaguzi uliowahi kufanyika nchini DRC Julai 30, 2006 walilalamikia kutengwa kushiriki upigaji kura wakidai wao ni binadamu na jamii isiwachukulie wa kama Nyani, nanukuu kauli ya Mbilikimo Kawaya Situka Fofana akisema, “Sisi ni Binadamu sio Nyani, tutambuane na tujumuishwe kwenye mambo ya msingi kijamii na pia tusitengwe”.

Mwanamitindo Maarufu ambaye ni Mbilikimo, Fatima Timbo.

Hata hivyo, mbali na makabila ya Wambilikimo, kuna watu katika makundi yoyote ya jamii ambao wanaweza kuwa wafupi kupita kiasi kwa sababu 300 na zaidi tofauti za kiafya na mtu wa namna hiyo kwa Kiingereza anaitwa dwarf huku Afrika Makabila ya Wambilikimo yakipatikana nchini Rwanda, Burundi, Uganda, DRC, Jamhuri ya Kongo – ROC, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Kamerun, Guinea ya Ikweta, Gabon, Angola, Botswana, Namibia, Madagaska na Zambia.

Maguri kuvunja rekodi Ligi Kuu 2023/24
De Bruyne kufanyiwa upasuaji