Kamanda wa Polisi wa Jimbo la Rivers nchini Nigeria, Friday Eboka amesema wamemkamata mshukiwa wa Reverend Sister, anayejulikana kama Maureen Wechinwu ambaye anadaiwa kuhusika katika wizi wa watoto.
Mtuhumiwa huyo, alifanyiwa Gwaride kati yake na washukiwa wengine 20 waliokamatwa katika jimbo hilo ndani kati ya mwezi Agosti na Septemba kwa makosa mbalimbali.
Amesema, Polisi pia waliwaokoa watoto kumi na watano kutoka kwa makazi yake yaliyopo katika Jumuiya ya Aluu eneo la Serikali ya Mtaa ya Ikwerre jimboni humo.
Eboka ameongeza kuwa, washukiwa wote 21 walitembezwa katika makao makuu ya kamandi huko Port Harcourt ambapo wahudumu wa Kitengo cha Ufuatiliaji cha CP kinachosimamia upelelezi walivamia makazi ya mshukiwa na kuwapata watoto hao.
Baadhi ya watoto hao, waliwasimulia Polisi jinsi walivyo “tekwa” na kupelekwa kwa mtuhumiwa huyo ambaye ni dada Mchungaji anayedaiwa kuwauzia wateja wake ndani na nje ya jimbo hilo.
Alisema “Mnamo tarehe 3 Septemba 2022, Operesheni ya Kurejesha Amani ya Askari wa Kamandi, wakitekeleza taarifa za kuaminika kuhusu maficho ya walanguzi wa watoto.”
Ameongeza kuwa, “Pia walivamia Omuigwe Abuja katika awamu ya pili huko Aluu, katika eneo la Serikali ya Mtaa wa Ikwerre ambako bibi mmoja aliyedai kuwa Mchungaji Dada, Maureen Wechinwu mwenye umri wa miaka 44 alikamatwa.
Katika operesheni hiyo, Watoto kumi na tano waliokolewa huku Maureen akikanusha tuhuma zote zinazomkabili, na kusema aliwahi kuwa Mchungaji nchini Uingereza.