Jumla ya watu sita (Watumishi wa Serikali ya Wilaya ya Kiteto, Manyara – Idara ya afya na Elimu), wamefariki na wengine saba kujeruhiwa baada ya kutokea kwa ajali ya magari kugongana uso kwa uso eneo la pori namba moja Wilayani Kiteto, Mkoani Manyara

Akisimulia tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mbaraka Batenga amesema ajali hiyo imehusisha gari la kubebea Wagonjwa (Ambulance) lililokuwa likitoka Kibaya (Kiteto), kugongana na gari dogo aina ya Totota Prado.

Ajali ya gari la wagonjwa lililochukua uhai wa watu sita.

Amesema, mara baada ya ajali hiyo majeruhi wapatao watano walipelekwa Hospitali jijini Dodoma kwa ajili ya matibabu na uangalizi huku majeruhi wawili wakibaki katika Hospitali ya Wilaya, Kiteto, huku Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, RPC. George Katabazi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema atatoa tarifa zaidi ikiwemo majina ya waliofariki hapo baadaye.

Eneo la tukio Prado na Gari la Wagonjwa baada ya kugongana.

Batenga amefafanua kuwa, “Gari la kituo cha afya cha Sunya lilikuwa likimpeleka mgonjwa Hospitali na baada ya kumshusha likiwa linarejea bahati mbaya likagonga uso kwa uso na gari aina ya Prado ambayo iliyokuwa ikitokea Kilindi (Tanga), kuja Kibaya (Kiteto).”

Madereva, Wafugaji waonywa uharibifu wa barabara
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Novemba 8, 2022