Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan, Imran Khan amesema maandamano ya kuipinga serikali kuelekea mji mkuu Islamabad yataendelea kesho Jumanne.

Maandamano hayo yalisitishwa katika wilaya ya Wazirabad mashariki mwa mkoa wa Punjab baada ya Khan kujeruhiwa kwa risasi katika jaribio la kutaka kumuua.

Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan, Imran Khan akiongea mara baada ya kutoka Hospitalini hapo jana Novemba 6, 2022. Picha ya Tribune India.

Akizungumza akiwa kwenye kiti cha magurudumu katika hospitali ya Shaukat Khanun alikokuwa amelazwa, Khan amerudia tena matakwa yake kutaka uchunguzi ufanywe kuhusu kushambuliwa kwa risasi.

Aidha, ametaka maafisa watatu wenye mamlaka makubwa serikalini na jeshini wajiuzulu, akidai walihusika kupanga shambulizi dhidi yake ambalo pia lilisababisha kifo cha mfuasi wake mmoja na wengine 13 kujeruhiwa.

Idadi ya watu Duniani kufikia Bil. 8
Polisi yapokea msaada wenye thamani ya mil. 30