Huenda Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Afrika Kusini Skudu Makudubela akawa sehemu ya mchezo wa Fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba SC kutokana majeraha aliyoyapata kutokuwa makubwa.

Hiyo ni baada ya kiungo huyo, kutolewa dakika ya saba ya mchezo wa Nusu Fainali wa Ngao ya Jamii waliocheza dhidi ya Azam FC kwenye Uwanja wa Mkwakwani Mkoani Tanga baada ya kuchezewa vibaya James Akaminko.

Katika mchezo huo, Young Africans walipata ushindi wa mabao 2-0 yaliyofungwa katika kipindi cha pili kupitia kwa Stephane Aziz Ki na Clement Mzize.

Akizungumza jijini Tanga Meneja wa Young Africans, Walter Harrison amesema: “Hali ya Skudu kwa sasa inaendelea vizuri na wala hakupata jeraha kubwa sana katika mchezo dhidi ya Azam FC baada ya kuangalia kwa kina jeraha lake.

“Kwa sasa yupo chini ya uangalizi wa jopo maalum la madaktari na anaweza akawepo katika mchezo wa fainali dhidi ya Simba SC kesho Jumapili japo sio kwa asilimia zote na kama atakosekana basi atapatikana katika michezo ijayo,” amesema kiongozi huyo.

Hofu yatanda uwanja wa Mkwakwani
Hofu yampanda Pep Guardiola