Rapper Jeffery Lamar Williams maarufu kama Young Thug ambaye amekuwa akiandamwa na kesi kila uchwao ameshtakiwa na duka linalofanya biashara ya vito vya thamani lijulikanalo kama Ice Box kwa madai kuwa ameshindwa kulipa kiasi cha dola $115 sawa na zaidi ya shilingi millioni 264 za kitanzania .
Wamesema kuwa rapper huyo alichukua vito vya thamani kwa makubaliano ya kulipa nusu halafu atamalizia lakini rapper huyo hakufanya hivyo na kusababisha duka hilo maarufu Ice Box kumshtaki na kumtaka alipe deni kama walivyo kubaliana kumalizia kiasi kilicho baki baada ya kulipa millioni 218.
Aidha Young Thug ameshindwa kulipa deni hilo licha ya juhudi za wanasheria wa kampuni hiyo kumtafuta.
Matthew Parish ambaye ni mwanasheria amesema kuwa walimuandikia barua October 16 mwaka huu kumtaka akamilishe kiasi hicho lakini mpaka sasa mambo yamekuwa kimya huku rapper huyo akiwa hatoi ushirikiano wowote mpaka sasa.
-
Kim Kardashian afunguka kuhusu video yake ya ngono
-
Meek Mill amapa ushauri Tekashi 69, ‘asijifanye mgumu’
-
TCRA yataja wamiliki wa Wasafi TV, Kusaga hakutajwa
Hata hivyo, Rapper huyo ambaye bado anakabiliwa na mashtaka 17 ya jinai kwa makosa ya kukutwa na dawa za kulevya na kumiliki silaha kinyume cha sheria mwaka 2017.