Kampuni ya Songas imeigawia serikali zaidi ya Sh11 bilioni kwa mwaka huu wa fedha kati ya Sh 30 bilioni ilizotenga kwaajili hiyo.
Fedha hizo zimelipwa kupitia mashirika ya umma yenye hisa Songas ambayo ni Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) lililopokea kiasi cha Sh 2.9 bilioni na Shirika la Maendeleo la Petroli Tanzania (TPDC) lililopata Sh8.9 bilioni.
Aidha, serikali pia itapokea kiasi cha Sh736 milioni kutoka katika mfuko wa maendeleo (TDFL) uliopokea gawio la kiasi cha Sh2.3 bilioni ambamo inamiliki asilimia 32 ya hisa zake.
Akipokea mfano wa hundi ya gawio hilo, mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Tanesco, Dkt. Alex Kyaruzi amesema kuwa gawio hilo limetolewa katika wakati muafaka kwani shirika hilo linahitaji fedha ili kuweka mambo yake sawa.
-
Tanzania na Ujerumani zatenga bilioni 375.4
-
Ujenzi wa machinjio ya kisasa ukamilike kabla ya Desemba- Mpina
-
Video: Lissu asimulia mambo mazito kwa dakika 60, Mchezo mchafu tena bandarini
“Tunavunja jengo letu na kuwahamisha watumishi, hivyo fedha hizi zilizotolewa zitasaidia pakubwa sana kufanikisha shughuli hii,”amesema Dkt. Kyaruzi