Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Jeanine Mabunda ameondolewa katika nafasi yake baada ya wabunge kupiga kura ya maoni dhidi yake iliyowasilishwa Bungeni na Upinzani.
Wabunge 281 kati ya 484 wa Bunge hilo wamemtaka kiongozi huyo aondoke kwenye nafasi hiyo katika kikao cha kupiga kura ya kumuondoa madarakani Spika wa bunge, Jeanine kutoka chama cha Joseph Kabila.
Upande wa Chama cha Rais mstaafu Joseph Kabila tayari kulikuwa na mzozo katika vyama vilivyokuwa vinamuunga mkono, hivyo hiyo inatajwa kuwa huenda ndiyo sababu ya kuanguka kwao.
Kwa sasa hatua inayofuata ni Waziri Mkuu kujiuzulu na Rais Felix Tshekedi kumchagua mtu atakayeunganisha vyama Bungeni kwa kuwa nia yake ni kuvunja muungano huo.
Hata hivyo swali linalowaumiza vichwa wengi, ni inakuwaje Spika huyo ashindwe kupata kura za kutosha kumtetea wakati Wabunge wa chama chake ndio wengi zaidi.