Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai amezitaka asasi za kiraia nchini kutoruhusu migongano, migogoro na kuzingatia kufanya kazi kwa Weledi kwa mustakabali wa taifa.


Spika Ndugai ameyasema hayo katika maadhimisho ya wiki ya asasi za kiraia AZAKI Jijini Dodoma ambapo amesema ni wakati wa asasi hizo kijitathimini na kufanya kazi kwa mujibu wa Sheria zinazowaongoza.


“Niwatake na niwaombe sana msiruhusu migangano na migogoro kwani kwakufanya hivyo kazi zenu zitaenda na zitakuwa na weled  wa hali ya juu,” Amesema Ndugai.

Amesema kuwa mbali na asasi za kiraia kutoa mchango mkubwa katika kujenga nchi lakini kukiwa na migogoro na migongano ndani ya asasi  itakuwa ni jambo gumu kufanikisha malengo au hazma mliyokiwekea.


Kwa upande wake Jenipher Kato  muwakilishi wa asasi ya Wote Sawa inayojishughulisha na Utoaji Elimu na Kutetea Wafanyakazi wa Majumbani amesema kuwa katika wiki ya asasi za kiraia wanatumia kuelimisha jamii kuhusu wafanyakazi wa majumbani ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya umuhimu wa kuwapa wafanyakazi wa ndani mikataba.


Wiki ya asasi za kiraia inafanyika Jijini Dodoma ambapo asasi mbalimbali zinapata nafasi ya kukutana na kujadili mambo yahusuyo asasi hizo pamoja na kutoa Elimu mbalimbali kwa jamii.

Wateule wa Rais waonywa
Rais Samia atoa maagizo kwa uongozi UWT