Makamu wa Rais wa Tanzania Dk Philip Isdory Mpango amewataka wateule wa Rais kufanya kazi kwa pamoja na ushirikiano kati ya Mawaziri, Naibu Mawaziri, Katibu wakuu na Naibu Katibu Wakuu katika Wizara zote.

Mpango meyasema hayo leo Ikulu jijini Dar es Salaam katika hafla fupi ya kuwaapisha viongozi waliobadilishiwa Wizara ambao ni Innocent Bashungwa na Pauline Gekul wa wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na makamishna wa Tume ya Uchaguzi.

“Ukiwa Kiongozi jitahidi kuwa Mnyenyekevu katika kazi yako, yeye anajua kwa nini amewateua na hivyo mfanye kazi kwa pamoja hakuna haja ya kunyanyua mabega. Nawaomba mchukue haya maneno kama onyo kutoka kwa msaidizi mkuu wa Rais na hatutarajii kutakua na mivutano na kazi itaendelea” amesema Mpango.

Nae waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika kutoa neno katika hafla hiyo ya uapisho amesema iliyokuwa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo imeonyesha mafanikio makubwa katika michezo mbalimbali yenye ushindani na timu za nchi nyinyine kimataifa na sasa itakapokua imejitegemea itaonyesha mafanikio makubwa zaidi.

Ameongeza kuwa Wizara mpya ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imepata mafanikio makubwa kwa kua inaendelea kukusanya wabunifu wengi ambao wanafanya ajira zao katika sekta ya TEHAMA.

“Juzi nilipata fursa ya kuwa Mgeni Rasmi katika Mkutano Mkuu wa Tano wa Mwaka huu 2021 ulokusanya watu wanaojihusisha na TEHAMA zaidi ya mia nane, Yako mafanikio makubwa yanayoonekana yanakuja hivyo kumpata Naibu waziri tunaamini anaenda kukamilisha nia yako ya Kuona eneo hili la TEHAMA linaimarika” ameongeza Majaliwa.

Nao Makamishna wa Tume ya Uchaguzi walioapishwa wametakiwa kuendelea kufanya kazi na kusimamia yale ambayo yanaratibiwa na Tume katika utaratibu uliopangwa na kuepusha migogoro.

Mfanyabiashara Mkubwa wa dawa za kulevya akamatwa Colombia
Spika Ndugai ateta na Asasi za kiraia