Spika wa Bunge Job Ndugai, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu duniani yatakayofanyika kimkoa wilayani Kongwa Dodoma, ambapo Sika atatumia nafasi hiyo kukabidhi vifaa visaidizi kwa watu wenye ulemavu.
Hayo yameelezwa na katibu wa Shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu( SHINYAWATA) Justus Ngw’atalima, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Ngw’antalima amesema kuwa jumla ya washiriki 500 kutoka vyama mbalimbali vya watu wenye ulemavu kutoka wilaya zote za mkoa wa Dodoma wanatarajiwa kushiriki ambapo maadhimisho haya yataanza Disemba 1, hadi Disemba 3 mwaka huu.
Aidha amesema kuwa pamoja na kuabidhi vifaa pia shughuli mbalimbali zitafanyika kwenye maadhimisho hayo ikiwa ni kutoa elimu kwa watu watakao shiriki.
”Ni mategemeo yetu kuwa kuona watu wenye ulemavu kuona watu wenye ulemavu wakipatiwa elimu na haki sawa kama ilivyo kwa wengine ambao hawana ulemavu wowote, siku hii tutakutana kwa pamoja na kujadili maana sisi tunashida nyingi ambazo zinahitaji msaada” amesema Ngw’ antalima.