Spika wa Bunge la Marekani, Nacy Pelosi ameitembelea nchi ya Taiwan ambapo anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo na rais wa Taifa hilo kabla ya kuondoka Agosti 3, 2022.

Spika Pelosi, amewasili katika eneo hilo licha ya kuwepo kwa katazo na vitisho kutoka China, na kwamba ziara hiyo ni ukiukwaji wa sera ya China ambayo inatambua Taiwan kama eneo la china.

Akizungumza na Naibu Spika wa Bunge la Taiwan, Tsai Chi-chang mara baada ya kuwasili, Pelosi alihalalisha ziara yake kwenye kisiwa hicho kwamba haivunji makubaliano yoyote kati ya China na Marekani, na kwamba lengo lake kuu ni kuonesha uungaji mkono wake kwa demokrasia ya Taiwan.

“Tunataka kuongeza ushirikiano na majadiliano baina ya Mabunge yetu, na tunafanya hivyo wakati rais wetu amependekeza mpango wa uhusiano wa Asia na Pasifiki, ambao tunauunga mkono na tunataka tuwe makini juu ya namna tunavyoshirikiana na Taiwan kwenye jambo hili.” Amesema Pelosi.

Kwa upande wake Rais, Tsai Ing-wen wa Taiwan amesema kisiwa hicho hakitayumbishwa na vitisho vya China ambayo imeamuwa kufanya mazoezi ya kijeshi karibu sana na kisiwa chao wakati huu wa ziara ya Spika Pelosi.

“Japo tunakabiliwa na vitisho vya hali ya juu vya kijeshi, Taiwan haitarudi nyuma. Tutaendelea na kushikilia uzi huu huu kwa ajili ya kuilinda demokrasia.” amesema Rais huyo.

Wizara ya mambo ya nje ya china imesema kuwa kitendo hicho ni kitakuwa na madhara makubwa katika msingi wa kisisa wa ushirikiano kati ya China na Marekani.

Ofisi ya Rais wa Taiwan imeeleza kwamba inaamini ziara hiyo itaimarisha uhusiano na Marekani na inalenga kuimarisha amani na utulivu katika ukanda huo wa bahari ya Pacific.

Mtuhumiwa mauaji ya Mwanafunzi UDSM akamatwa
Odinga aongoza kura za maoni