Sakata la Kampuni ya kushashiri ya SportPesa na Klabu ya Young Africans limemuibua Mchambuzi wa Soka la Bongo Jemedari Said Kazumari, akihoji taratibu zilizochukuliwa na Uongozi wa Klabu hiyo, hadi kufikia hatua ya kukiuka makubaliano na Wadhamini wao.
Young Africans juzi Jumatatu (Januari 30) ilisaini mkataba na kampuni ya Haier wenye thamani ya Tsh bilion 1.5 kama mdhamini mkuu wa Kombe la shirikisho Barani Afrika Hatua ya Makundi msimu huu.
Jemedari ametumia Kurasa zake za Mitandao ya Kijamii akiandika: “Taarifa hii kutoka SPORTPESA ina kamilisha tu maoni yetu kwamba Yanga SC inaongozwa “KISHIKAJI”. bila kufuata weledi wala utawala bora.
Klabu yenye viongozi imara wenye kufanyakazi kwa kufuata miiko ya uongozi haiwezi kujiingiza kwenye mambo ya KIHUNI kama haya.
Huwa najiulizaga maswali hivi kweli Yanga SC ina idara ya sheria? Kazi yake hasa nini? Mbona kila uchao Yanga wanaingia kwenye mgogoro wa kisheria (kimkataba). Morisson, Feisal, Sportpesa ni mifano tu, yako mengi.
Klabu ishachukua pesa ya SPORTPESA halafu inaenda kuchukua pesa HAIER kwajili ya kitu hicho hicho halafu kwa kuingia mikataba, bado kuna idara ya sheria ya klabu? Huyo mwanasheria kazi yake nini?
Rais wa Yanga SC ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM mpaka leo, Kampuni ya HAIER ni kampuni ambayo ni mshirika mkubwa wa GSM hapa Tanzania, wanapotaka kuitumia Yanga SC kuwekeza Rais wa klabu anasema nini.
Ndiyo maana anashindwa kufuata makataba wa Sportpesa anaamua kuingia wa haier kwakuwa unagusa maslahi yake ya kazini.
Tulikuwa maadui wakati tunatoa maoni ya mgongano wa kimaslahi kumhusu Rais wa klabu tukaitwa majina yote. Lakini hiki ndicho hasa ilikuwa maono yetu. Leo Yanga SC ndiyo hatakama madai itadaiwa klabu, hawa watu wanaweza hata kesho wakaondoka ila klabu itabaki inadaiwa kwa kushindwa kufuata matakwa ya kimkataba.
Bodi ya Wakurugenzi wa Yanga SC walipitishaje hii kitu? Bodi ambayo Makamu wake ni CEO wa Zanzibar Insurance Corporation unaetegemea ajue mambo ya mikataba ya kibiashara akasimama upande wa klabu kwakuwa Rais wake tayari ana maslahi na upande wa pili, lakini naye ni walewale tu, wakute mtandaoni sasa ngebe nyiingi.