Mamlaka ya Usimamizi wa sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) inawataka wanachama wote wa mifuko ya HIfadhi ya Jamii kuhakikisha wana vitambulisho vya taiafa (National Identity Card). Kwani kupitia kitambulsiho cha Taifa mwanachama ataweza kupata huduma na taarifa zake zote muhimu zinazohusiana na masuala ya Hifadhi za jamii kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

Ambapo Vitambulisho hivyo vya Taifa vinatolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA kwenye ofisi zake zilizopo kote nchini, ili kupata kitambulisho cha Taifa mwanachama anatakiwa awe na nyaraka au vielelezo vifuatavyo.

Cheti cha kuzaliwa, Pasi ya kusafiria, Vyeti vya Shule msingi na sekondari,, Leseni ya udereva, kadi ya bima ya afya, Kadi ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii, Kitambulisho cha Mzanzibar Mkaazi, Kitambulisho cha kupiga kura na kitambulisho cha Kazi.

Pia mwanachama anatakiwa kuzingatia kanuni na taratibu za usajili kama zinavyoelekezwa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kupitia tovuti ya NIDA ambayo ni www.nida.go.tz

Aidha kwa maelezo zaidi imetoa mawasiliano katika Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa sekta ya Hifadhi ya jamii (SSRA), kupitia namba 0656 631253 au 0715 44 67 21 au kwa barua pepe info @ssra.go.tz au fika ofisin i kwao Dodoma jengo  la Mkaguzi Mkuu wa Serikali au Dar es salaam katika jengo la Alpha barabara ya Bagamoyo.

TCRA yapiga 'stop' mitandao isiyojisajili kuhabarisha, Jamii Forum yatii amri
Merkel amkosoa vikali Donald Trump