Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utmishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki amezielekeza Taasisi za Serikali kuandaa Mpango wa Mafunzo kwa watumishi kwa njia ya uwazi na shirikishi ili kuepuka malalamiko kutoka kwa baadhi ya watumishi wa umma.
Ameyasema hayo mapema hii leo katika kikao wa watumishi wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam, ambapo maesema kuwa mwajiri anapoandaa Mpango wa Mafunzo kwa watumishi wake ni vyema mpango huo ukawa shirikisha watumishi wote ili kujua mpangilio wake.
Amesema kuwa Mpango wa Mafunzo shirikishi utasaidia kuondoa malalamiko, utasaidia pia kutorudisha fedha zilizobaki kwa watumishi wa umma ambao walipangwa lakini wakashindwa kuhudhuria mafunzo kwa sababu mbalimbali.
“Napokea malalamiko mengi sana kuhusiana na upendeleo katika suala la mafunzo, napenda kuwasisitiza waajiri tuandae Mpango wa Mafunzo ambao ni shirikishi kwa watumishi wote kuepuka haya, wengine wanapangwa na hawashiriki mafunzo,”amesema Kairuki
Aidha, ameongeza kuwa sababu ya kutoshirikishwa wapo wanaopotosha kuwa Serikali imefuta Mpango wa Mafunzo kitu ambacho si cha kweli na amewahakikishia watumishi hao kuwa Serikali haijafuta mafunzo.
-
Jafo ang’aka, awataka maafisa elimu kuboresha mazingira ya shule nchini
-
RC Rukwa atoa tahadhari kwa wasimamizi wa fedha za ukarabati shule Kongwe
-
RC Singida awapa somo watumishi wa umma, awataka wapunguze muda wa vikao
Hata hivyo, Kairuki yupo katika ziara ya kikazi katika Mkoa wa Dar es salaama ambapo leo ni siku ya nane akiwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kwa kukutana na watumishi wa umma wa kada zote katika vikao kazi.