Taasisi mbalimbali nchini, zimetekeleza maelekezo ya Serikali kuhusu kusitisha matumizi ya kuni na mkaa kwa ajili ya kupikia ikiwemo Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Jeshi la Magereza kuwa na utayari wa kusitisha matumizi ya kuni na mkaa, ikiwa ni hatua ya kupunguza ukataji wa miti ambao ni chanzi cha uharibifu wa mazingira.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Khamis Hamza Khamis wakati akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (2021 – 2026) kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira jijini Dodoma.

Amesema, kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, hadi kufikia wiki hii, vyuo 30 kati ya 35 vilivyopo hapa nchini vimeanza kutekeleza maelekezo hayo kwa kuanza kutumia nishati mbadala na hayamuhusu Mwananchi mmoja mmoja bali yanazilenga taasisi zinazolisha watu zaidi ya 100.

Khamis ameongeza kuwa, katazo la matumizi ya kuni na mkaa limelenga kuhifadhi mazingira na kwamba linatokana na maazimio ya Kamati ya Kitaifa ya Nishati Salama ambapo kila taasisi ilipewa majukumu na Serikali inatekeleza katazo la kuni na mkaa na kuingia katika matumizi ya nishati safi ya kupikia, ili kuepusha uharibifu wa mazingira.

Kuhusu Mkakati wa Mkakati wa Taifa wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (2021 – 2026), Naibu Waziri Khamis amesema una lengo la kujenga uwezo wa kitaifa wa kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi na kuwezesha nchi kutumia njia zenye uzalishaji mdogo wa gesijoto katika kufikia maendeleo endelevu.

Amesema kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati imeandaliwa Dira na Mkakati wa Nishati Safi ya Kupikia pamoja na kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa jamii yote ya Watanzania kwa lengo la kunusuru mazingira
yasiharibike.

Ahmed Ally: Tumeionesha Afrika Simba ni nani
TAFIRI kuja na mfumo rasmi taarifa za Uvuvi