Shirika la afya Duniani (WHO), limeonya kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu unaoendelea kuripotiwa kwenye mataifa huku nchi za Malawi, Syria na Lebanon, zikitajwa kuathirika zaidi.

Kufuatia hatua hiyo, Mkurugenzi wa shirika hilo, Dkt. Tedros Adhanom amewataka wakuu wa nchi ulimwenguni kuchukua tahadhari ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na uhaba wa chanjo za ugonjwa huo.

Mkurugenzi wa Shirika la Afya Ulimwenguni WHO, Dkt. Tedros Adhanom.

Amesema, “Tangu mwezi Januari mwaka jana (2022), Mataifa 31 ambayo ni sawa na asilimia 50 kwa zaidi ya miaka iliyopita yameathiriwa na Maradhi mbalimbali hivyo tujitahidi kuchukua tahadhari.”

Hata hivyo, WHO pia imetoa wito kwa mataifa duniani kuwasisitizia raia wake umakini na matumizi ya barakoa haswa wanaposafiri safari za muda mrefu ili kukabiliana na maambukizi ya maradhi mbalimbali ikiwemo Uviko-19 aina ya Omicron.

ASFC: Hatua ya 32 Bora hadharani
Dodoma jiji FC: Haikuwa rahisi kumsajili Sey