Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’ leo Ijumaa (Januari 13) limepanga Droo ya Hatua ya 32 ya Kombe la Shiriskiho ‘ASFC’, huku Mabingwa watetezi Young Africans wakipangwa na Rhino Rangers ya Tabora.

Mwanafainali mwingine wa Msimu uliopita Coastal Union amepangwa kukutana Simba SC, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, huku Azam FC ikiikaribisha Dodoma Jiji FC, Uwanja wa Azam Complex.

Singida Big Stars itasalia nyumbani Uwanja wa Liti mkoani Singida kuikabili Ruvu shooting itakayofunga safari kutoka Mkoani Pwani.

Ratiba ya Michezo mingine ya Hatua ya 32 Bora ASFC.

Michezo ya Hatua ya 32 Bora imepangwa kuchezwa kati ya Januari 27 hadi 29-2023.

Utitiri wa kodi waliza Wafanyabiashara
Tahadhari yatolewa mlipuko wa kipindupindu