Wakati Wafanyabiashara na wawekezaji wakilalamika mfumo wa kodi uliopo nchini kuuwa biashara, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba amesisitiza kuwa lengo la Serikali si kuwaumiza walipa kodi.

Hayo yamejiri wakati wa kongamano la kitaifa la kodi, ambapo maeneo yaliyolalamikiwa ni pamoja na msamaha wa Kodi ya ongezeko la Thamani (VAT), na kutozingatiwa kwa itifaki ya kodi ya Afrika Mashariki.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba.

Mwakilishi wa wadau wa usafiri na usafirishaji wa anga, Latifa Sykes akizungumza katika Kongamano hilo alisema, hatua ya Serikali kuondoa msamaha wa VAT kwa ndege za kukodi imesababisha ndege za nchi nyingine kuvamia soko la Tanzania.

Kwa upende wake, Waziri Mwigulu alisema tofauti na hali ilivyokuwa kabla na baada ya uhuru, Serikali itaendelea kuwalinda wazalishaji kwani ni washirika wakuu katika ufanikishaji wa maendeleo nchini.

Kisonono waibuka kwa kasi, tahadhari yatolewa
ASFC: Hatua ya 32 Bora hadharani